Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), George Simbachawene, ameiagiza Jumuiya ya Wadau wa Nishati Jadidifu Tanzania (TAREA) kufanya utafiti katika Jiji la Dar es Salaam ili kubaini kiasi cha matumizi ya nishati jadidifu.
Alitoa agizo hilo wakati akifungua Maonesho ya 14 ya Kitaifa ya Siku ya Nishati Jadidifu yaliyofanyika Mnazi Mmoja, Dar es Salaam yakiwa na kauli mbiu: “NISHATI JADIDIFU KUFIKIA TANZANIA YA VIWANDA 2025” yaliyoandaliwa na TAREA na kufanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar Salaam.
Aidha, ameyataka mataifa yaliyoendelea kuacha kuleta bidhaa chakavu za kielektroniki zikiwamo runinga na friji katika nchi zinazoendelea ikiwamo Tanzania kuacha kwa kuwa ni majanga.
Alikuwa akijibu risala ya TAREA iliyosomwa kwake na Makamu Mwenyekiti wa TAREA, Mhandisi Prosper Magali aliyesema licha ya TAREA na wadau mbalimbali kuhamisisha matumizi teknolojia ya nishati jadidifu, zipo changamoto kubwa za kudhibiti taka zitokanazo na bidhaa za kielektroniki zikiwamo runinga na friji.
Simbachawene alisema inasikitisha kuona vifaa vilivyotumika na kuchakaa katika mataifa yaliyoendelea bado zikiwamo friji na TV bado zinaletwa katika mataifa yaliyoendelea ikiwamo Tanzania.
Akasema: “Kwa nchi zilizoendelea, kama kitu ni kibaya, tusikitumie wote; tusione ni kibaya tukapeleka Afrika maana madhara yake tabaka la ozini ni makubwa. Uchafuzi wa hali ya hewa husababisha kumomonyoka kwa tabaka la ozoni na kubadilika kwa tabianchi huathiri watui wote.”
Alisema serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira, imeandaa kanuni mpya za udhibiti na usimamizi wa taka hatarishi za mwaka 2019 zilizoanza kutumika Septemba mwaka huu.
“Kanuni hizi zinasimamia taka hatarishi mbalimbali zikiwamo betri chakavu, hivyo serikali inawahakikishia kuwa itaendelea kusimamia kanuni hizo ipsavyo ili kudhibiti uchafuzi unaoweza kutokea na utupaji usio salama,” alisema na kuongeza kuwa, matumizi ya niashati ya kuaminika na endelevu hayaepukiki kwa maendeleo ya taifa na kuelekea uchumi wa viwanda ifikapo mwaka 2025.
Simbachawene alisema: “Mafanikio katika sekta zote za uchumi, huduma za jamii na maendeleo yanategemea upatikanaji wa kuaminika na endelevu wa nishati ya kutosha usiokuwa na madhara katika mazingira.”
Alisema sekta ya viwanda kutumia fursa hiyo kujipatia umeme katika vyanzo vya nishati safi na nafuu kwa shughuli za viwanda kwa mifumo na kazi kama kuchemsha mahji, kuvuta maji kwa ajili ya umwagiliaji na majiko sanifu kwa taasisi za umama kama shule na majeshi.
“Natoa mwito kwa taasisi za umma kama majeshi, magereza, hospitali, shule na vyuo kuingia katika matumizi ya teknolojia ya nishati jadidifu maana miti mingi inakatwa na magereza na shule hivyo, uharibifu wa mazingira ni mkubwa,” alisema
Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Jeroen Verheul alisema ili teknolojia ya nishati jadidifu isambae na kutumika zaidi kwa umma, lazima kuwepo mazingira rafiki zaidi ya kisera na kisheria na kwamba, sula hjili linahitahji ubia wa dhati.
Alisema nchi yake itaendelea kushitrikiana na Tanzania katika kusaidia matumizi ya teknolojia ya nishati jadidifu am,bayo ni msaada katika mapambano ya kidunia dhidi ya majanga yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi.
Awali, Mhandisi Magali ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa TAREA na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya maonesho hayo, alimwambia waziri kuwa, licha ya TAREA na wadau mbalimbali kuhamisisha matuimizi yteknolojia ya nishati jadidifu, zipo changamoto kubwa za kudhibiti taka zitokanazo na bidhaa za kielektrponiki zikiwamo runinga na friji.
“Taka za kielektroniki zimeendelea kuongezeka na tupo kwenye hatari kubwa ya uchafuzi wa mazingira kupitia taka hizi,” alisema magali.
Akaongeza: “Tunaomba Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira kukamilisha utungaji wa sheria za kusimamia biashara ya taka za kielektroniki ili kuwezesha shughuli za urejelezaji wa taka hizo ili kuhifadhi mazingira”.
Social Plugin