Klabu ya Aston Villa ya England, imetangaza kumsajili mshambuliaji wa kimataifa kutoka Tanzania Mbwana Samatta.
Usajili wa Mbwana Samatta unatarajiwa kuimarisha safu ya mashambulizi ya timu ya Aston Villa ambayo imekuwa ikilegalega katika ligi ya Premier.
Aston Villa imecheza mechi zake tatu zilizopita bila mshambuliaji wa kutambuliwa baada ya mshambuliaji wao raia wa Brazil Wesley Moraes kujeruhiwa hivyo kutoweza kucheza tena msimu huu.
Samatta aliyekuwa akiichezea klabu ya Genk nchini Ubelgiji, amefunga mabao kumi katika mechi zote likiwemo bao alofunga dhidi ya Liverpoool katika ligi ya Mabingwa uwanjani Anfield
Yeye ndiye mchezaji wa kwanza kutoka Tanzania kuwahi kusajiliwa na timu katika ligi ya Premier.
Social Plugin