LUCY Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga leo ameiongoza timu yake kupoteza kwenye mechi yake ya pili kwa kufungwa bao 1-0 na Azam FC, Uwanja wa Taifa.
Mchezo wa leo ambao ulichezwa huku mvua ikinyesha kipindi cha kwanza, ulikuwa na ushindani kwa timu zote ila mwisho wa siku Azam FC wakasepa na pointi zote tatu.
Bao pekee la ushindi la Azam FC lilipatikana kupitia kwa Ally Mtoni 'Sonso' aliyejifunga katika harakati za kuokoa mpira uliopanguliwa na mlinda mlango Faruk Shikalo kutokana na kona iliyopigwa na Bruce Kangwa.
Mchezo wa kwanza kwa Eymael aliyechukua mikoba ya Mwinyi Zahera kufungwa ulikuwa dhidi ya Kagera Sugar ambapo alifungwa mabao 3-0.
Juma Abdul, nahodha msaidizi wa Yanga amesema kuwa walijipanga kupata matokeo mazuri ila bahati haikuwa yao, mashabiki waendelee kuwapa sapoti.
Sure Boy wa Azam FC amesema kuwa wamepata matokeo hayo kutokana na kufuata maelekezo ya mwalimu.
Ushindi huo unaifanya Yanga isalie na pointi 25 ikiwa imecheza mechi 14 huku Azam FC ikijiongezea jumla ya pointi 32 nafasi ya pili
Social Plugin