Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mara kitamhoji aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, Kangi Lugola baada ya kutuhumiwa kuhusika katika mkataba wenye harufu ya ufisadi uliosababisha Rais John Magufuli kutengua uteuzi wake.
Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Mara, Samwel Kiboye amesema Lugola ambaye ni mbunge wa Mwibara atahojiwa na kamati ya maadili ya CCM mkoani humo.
Amesema Lugola kuhojiwa hakuhusiani na na taarifa ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ambayo itamhoji kesho Ijumaa Januari 31, 2020.
Kiboye amesema vitendo vinavyodaiwa kufanywa na Lugola vimemfedhehesha Rais Magufuli ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM.
Social Plugin