-
Mkuu
wa Mkoa wa Singida, Mhe. Dkt. Rehema Nchimbi, akiwahutubia watumishi wa Umma wa
mkoa wa Singida leo.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe.
Kassim Majaliwa Majaliwa, akiangalia jinsi mkorosho wa miaka 2 ulivyotoa
korosho katika shamba la pamoja (block
farming) wilayani Manyoni alivyotembelea Mkoa wa Singida hivi karibuni. Mhe.
Majaliwa alipongeza ubunifu huu uliofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Singida
ambapo hadi sasa takribani hekta 12000
zimepandwa mikorosho na hakuna mkoa wowote hapa nchini ambao umebuni mfumo huu kwenye zao lolote.
Na John Mapepele
Mkuu wa Mkoa wa Singida
Dk. Rehema Nchimbi amesema kuwa kila
mtumishi wa Serikali katika mkoa wake kuanzia mwaka huu 2020
atatakiwa kuonyesha mafanikio yanayotokana na
mishahara wanayolipwa na Serikali kupitia kauli mbiu maalum iliyoandaliwa na mkoa ya “mshahara wangu upo wapi” ifikapo mwisho wa mwaka huu.
Pia aliwaonya kuachana na mambo ya siasa
na badala yake kufanya kazi kwa bidii ili kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa Rais John Pombe Magufuli.
Akizungumza na watumishi
wa Umma wa mkoa wa Singida katika
mkutano maalum wa kwanza katika mwaka
huu 2020 mjini Singida leo ambapo Dk. Nchimbi alisema mkoa huo umeamua kuiishi
kauli mbiu hii baada ya kuona mafanikio ya kupigiwa mfano yaliyopatikana kutoka
kwa wanufaika wa mpango wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ulilenga
katika kunusuru kaya masikini na baada ya muda wa mradi waweze
kusimama wenyewe uliozinduliwa Septemba, 2014 mkoani hapo na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa.
Alisema katika mpango huo ruzuku ya shilingi elfu
ishirini(20,000/=) ilitolewa kwenye kila Kaya yenye sifa katika Halmashauri 6
kati ya 7 za mkoa pamoja na fedha za masharti ya afya na elimu ambayo kila kaya yenye mtoto anayesoma Shule ya
Msingi na Sekondari na wale chini ya miaka 5 walipewa kuanzia shilingi elfu mbili(2000) hadi elfu
sita (6000), ambapo alisema ruzuku hiyo imekuwa
msaada mkubwa kwa kaya masikini katika kuwanunulia sare, madaftari pamoja na kulipia matibabu
hasa kujiunga Mfuko wa Bima ya Afya ya
Jamii(NHIF).
Aliongeza kuwa hadi
kufikia mwezi Januari 2020, jumla ya
kaya 38,136 kutoka katika vijiji 278 zinanufaika na ruzuku hii na jumla ya shilingi takribani bilioni thelathini na saba na
milioni mia tisa (37,900,000,000) ziliwafikia walengwa.
“Napenda kuwahakikishia
kuwa hakuna kipindi ambacho watumishi wa
umma watakuwa na maisha bora kama hiki
kwa kuwa Serikali ya awamu ya Tano imeshaboresha kwenye kila sekta kama
miundombinu,huduma za afya, elimu itashindwaje kuboresha maisha ya watumishi
umma” alihoji Dk. Nchimbi huku akisisitiza kuwa watumishi wazembe hawatavuka
mwaka 2020 wataondolewa mara moja kupisha watumishi wanaoendana na kauli mbiu
ya hapa kazi tu.
Aidha Dk. Nchimbi alisema
pamoja na kuhakikisha kuwa mishashara ya watumishi inaleta tija kwenye familia
na kuboresha uchumi, tayari mkoa unatekeleza
mikakati mahususi ya kilimo cha
kisasa cha pamoja cha zao la korosho kwa
wananchi wa Mkoa wa Singida ambapo ametoa rai kwa watumishi na wananchi
kujitokeza ili kupatiwa maeneo hayo ili kuyaendeleza kwa pamoja.
“Hadi sasa Singida siyo,
masikini, kame wala yenye njaa kama iliyokuwa ikitafsiriwa na baadhi ya watu
hapo awali. Tayari hekta elfu kumi na mbili (12000) za kilimo cha pamoja (block farming)
zimepandwa mikorosho na zimeanza kuzaa korosho katika Wilaya ya Manyoni.
Ninatoa shukrani na pongezi zangu za dhati
kwa Rais John Pombe Magufuli kwa kutupatia pikipiki 10 ili ziweze kusaidia
katika kazi hii” alisisitiza Dk.Nchimbi
Alisema kutokana na tafiti
zilizofanyika hivi karibuni zimeonyesha kuwa ardhi ya mkoa wa Singida ina ubora
mkubwa wa kusitawisha zao la Korosho kwa muda mfupi ukilinganisha na maeneo
mengi hapa nchini hivyo hakuna sababu ya watumishi na wananchi kutochangamkia fursa hiyo adimu
ambapo pia alionya kuwa wananchi ambao watabainika kuwa hawapo makini
wataondolewa katika program hiyo.
Social Plugin