Waziri wa Madini Doto Biteko kushoto akizungumza kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Sanare
Waziri wa Madini Doto Biteko katikati akizungumza,
kushoto ni Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro
Loata Sanare wakiwa kwenye kikao.
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akizungumza
Waziri
Biteko ameagiza uongozi wa Mkoawa Morogoro kwa kushirikiana na Wizara ya Madini kuandaa
maonesho ya madini kwalengo la kuelimisha Umma kwa watu wa Morogoro na mikoa jirani
juu yaSheria, Kanuni na fursa zilizopo katika Sekta ya Madini.
Hayo yamebainishwa leo
January 08, 2020 na Waziri wa Madini Doto Biteko alipofanya kikao na MkuuwaMkoawa
Morogoro, LoataSanare, kilichofanyika katika ukumbi wa WizarayaMadini, Mtumba Jijini
Dodoma.
“Nichukue
fursa hii kuwaelekeza wataalamu wote wa Wizara ya Madini na Taasisi zake kuhakikisha
wanashirikiana naMkoa wa Morogoro kuzitangaza fursa zinazopatikana katika Sekta
ya Madini Mkoani Morogoro kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo kuandaa maonesho yatakayopelekea
kuelimika kwa wananchi wa Mkoa huo,” alisema Waziri Biteko.
Aidha,
Waziri Biteko amesisitiza ushirikiano katika kusimamia Sekta ya Madini kati yaWizara
na Mkoa wa Morogoro na kumpongeza Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Morogoro Emmanuel
Shija kwa kazi nzuri anazozifanya katika ukusanyaji wa mapato ya serikali.
Waziri
Biteko amesema maendeleo ya Sekta ya Madini katika Mkoa wa Morogoro yatatokana na
wachimbaji wenyewe, hivyo Wizara na Mkoa inapaswa kuwalinda nakuwalea wachimbaji
na wadau wote wa madini mkoanihumo.
Akizungumzia
changamoto inayowakabili wananchi wa Morogoro Biteko alisema ni pamoja na uelewa
mdogo walionao juu ya masuala yanayohusiana na Sekta ya Madini kuwa ni kikwazo katika
kupelekea maendeleo Mkoani humo.
Kwa
upande wake,Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, ameonesha kufurahishwa na kitendo
cha Mkoa wa Morogoro kuonesha mafanikio makubwa katika makusanyo ya mapato ya serikali
kutoka shilingi 811,714,294.12 kwa mwaka 2017/2018 mpaka kufikia
1,031,865,068.41 kwamwaka 2018/2019.
“Madini
ya Ujenzi, Vito na Dhahabu tukiyasimamia vizuri hakika yatatuingizia fedha nyingi
watu wa Morogoro, hivyo nikuombe Mkuu wa Mkoa ukalifanyie kazi hilo, pia sisi kama
Wizara ya Madini tutashirikana na Mkoawa Morogoro kuhakikisha wawekezaji wanakuja
kuwekeza katika Sekta ya Madini Mkoani Morogoro,”alisemaNyongo.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Loata Sanare, amemuomba Waziri kupatiwa ushirikiano
katika kuitangaza Morogoro kuwani Mkoa wa Madini na sio kilimo peke yake.
Pia
Sanare, amesema, Mkoawa Morogoro una mpango wakufufua viwanda vya Ceramics
vilivyokuwepo ili kuongeza matumizi ya madini ya viwandani yanayopatikana katika
Mkoa huo kwa wingi na kuendeleza uhamasishaji wa uanzishwaji wa viwanda vipya vya
Ceramics.
Wakatihuohuo,
AfisaMadiniMkaziwaMkoawa Morogoro, Emmanuel Shija,amesema Mkoawa Morogoro una Jumlaya
leseni 3082 za wachimbaji wa dogo kati yake ni leseni 250 tu ndizo zinafanya kazi
ya uzalishaji, hivyo Ofisi ya Madini inaendelea na zoezi la kufuta leseni zote zenye
makosa.
“Mwaka
2019 jumlayaleseni 223 zilifutwa na jumla ya hati za makosa kwa leseni 836
zimetolewa, leseni hizo ziko kwenye utaratibu wa kufutwa ndani ya mwaka huu wa fedha
endapo wamiliki wa leseni hizo hawatarekebisha makosa yao kama Sheria inavyoelekeza,”
alisemaShija.
Kikao
hicho kilicho lenga kujadili changamoto na maendeleo ya Sekta ya Madini kwaMkoa
wa Morogoro ikiwa ni pamoja na kuangalia fursa zilizopo katika Sekta ya Madini katika
kuharakisha maendeleo ya mkoa huo.
Ambacho kilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Wizara
ya Madini na Taasisi zilizo chini ya Wizara akiwepo Naibu Waziri waMadini, StanslausNyongo,
Mtendaji Mkuu wa Tume ya Madini Prof. ShukraniManya, Mkurugenzi Taasisi ya Jiolojia
na Utafiti Tanzania Dkt Musa Budeba, Kamishna wa Madini Mhandisi David Mulabwa,
Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara ya Madini Edwin Egenge, Mkurugenzi wa
Sera na Mipango wa Wizara ya Madini Augustine Ollal na wengine.
Social Plugin