Watu zaidi ya saba wamejeruhiwa baada ya gari aina ya Hiace yenye namba za usajili T 836 DEB ikitokea Kishapu kwenda Shinyanga Mjini kumgonga mwendesha baiskeli na kutumbukia mtaroni wakati ikikwepa gari aina ya Toyota Harrier yenye namba za usajili T726 DFM.
Ajali hiyo imetokea majira ya saa 12 jioni leo Alhamis Januari 2,2020 katika eneo la Pepsi ‘Ushirika’ barabara ya Shinyanga – Mwanza.
Kwa Mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wameiambia Malunde 1 blog kuwa dereva wa Hiace akitokea Kishapu alikuwa anajaribu kumkwepa dereva wa gari aina ya Toyota Harrier aliyeingia kwenye njia isiyo yake ndipo Hiace ikamgonga mwendesha baiskeli ambaye ni miongoni mwa waliojeruhiwa wakiwemo wale waliokuwa ndani ya Hiace na wamekimbizwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya matibabu.
Inaelezwa watu saba wamekimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu
Inaelezwa watu saba wamekimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu
Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga likiongozwa na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Shinyanga (RTO) Anthony Gwandu wamefika eneo la tukio na tayari gari aina ya Harrier inashikiliwa katika kituo cha polisi.
Gari aina ya Hiace yenye namba za usajili T 836 DEB ikiwa kwenye mtaro baada ya kupata ajali kwa kumgonga mwendesha baiskeli na kutumbukia mtaroni wakati ikikwepa gari aina ya Toyota Harrier yenye namba za usajili T726 DFM katika eneo la Ushirika barabara ya Shinyanga - Mwanza- Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Gari aina ya Hiace yenye namba za usajili T 836 DEB na baiskeli eneo la ajali.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Social Plugin