Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

HUDUMA ZA FEDHA KWA NJIA YA SIMU ZINAVYOSAIDIA KUKUZA UCHUMI NCHINI


Katika siku za hivi karibuni huduma ya kutuma fedha, kupokea na kulipa kupitia simu za mkononi imekuwa jambo kubwa nchini na kwa kiasi kikubwa kichocheo cha maendeleo yetu. 

Tafiti nyingi zinaonyesha kuwa faida zinazohusiana na huduma za kifedha kwa njia ya simu za mkononi zinachangia sana kwenye kubadilisha nchi yetu kidijitali na kutusaidia kufikia malengo ya maendeleo kuelekea mwaka 2025. 

Huduma hii imewezesha watu wengi zaidi katika mfumo rasmi wa kifedha (financial inclusion). Imewapa njia rahisi na ya hakika wananchi wa kawaida na biashara kuweka akiba, kuwekeza, kutuma, kutoa na huduma nyingine lukuki ambazo sote sasa tunazitumia kidijitali. Kwa wafanyabiashara wadogo na wakati imewasaidia kukua zaidi, kukuza mtaji na kuongeza uwekezaji na ajira. 

Licha ya maendeleo haya, bado wako ambao huduma hizi rasmi za kifedha na mitaji hazijawafikia. Hatua inayofuata sasa ni kuhakikisha wale wote ambao hawajafikiwa na matunda haya ya maendeleo nao wanayapata na huduma ya fedha kwa njia ya simu ni njia muhimu na kuu zaidi kufikia watu hawa. 

Kukua zaidi kwa huduma hii kunategemea msingi mzuri wa uwekezaji katika sekta ya mawasiliano ya simu na mazingira mazuri ya kufanya biashara.  

Tuungane pamoja kuendelea kuipa nguvu sekta ya mawasiliano ya simu ili iendelee kutanuka zaidi ili sote tufaidi matunda yake. Miezi michache iliyopita kampuni mbili za Tigo na Zantel zimeunganisha shughuli zao. 

Hii ni hatua mojawapo ya kuboresha soko na kutoa huduma bora zaidi kwa taifa. Tukianza mwaka huu mpya wa 2020 tuendelee kutumaini kwamba sekta hii itaendelea kuwa bunifu ili kusukuma mbele dira ya maendeleo ya nchi kuelekea mwaka 2025.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com