Jeshi la Polisi mkoani Kigoma nchini Tanzania limezuia mkutano wa hadhara wa Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe uliopangwa kufanyika leo Ijumaa Januari 17,2020.
Kwa mujibu barua iliyoandikwa na jana Alhamisi Januari 16, 2020 na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kigoma M.R Mayunga iliuzungumzia mkutano huo wa Zitto ikisema kutokana na mazingira ya kiusalama unapaswa kusitishwa.
“Napenda kukujulisha kuwa mkutano umezuiliwa kwa tarehe uliyoomba kwa sababu za kiusalama kutokana na taarifa za kitentejensia zilizopo. Kwa hiyo hairuhusiwi kufanya au kuendelea na maandalizi ya mkutano,” ilieleza sehemu ya barua hiyo.
(2/3) Kwenye barua yao kwa Ofisi ya Mbunge huyo, Jeshi la Polisi Wilaya ya Kigoma linadai kuwa limezuia mkutano huo "..kwa sababu za kiusalama kutokana na taarifa za kiintelijensia zilizopo". #KigomaYaZambarau pic.twitter.com/BxosQjkeMu— ACT Wazalendo (@ACTwazalendo) January 17, 2020
Social Plugin