JESHI LA SUDAN LAZIMA JARIBIO LA MAPINDUZI


Jeshi la Sudan linayashikilia makao makuu ya kikosi cha usalama wa taifa cha nchi hiyo ambacho awali kilikuwa kitiifu kwa rais aliyepinduliwa Omar al-Bashir, ripoti zinaeleza.

Mapambano yalianza Jumanne katika jiji la Khartoum ambapo milio ya milipuko ilisikika. Kitengo hicho cha usalama wa taofa kwa sasa kinavunjwa.

Serikali inaadai kuwa uasi huo umechochewa na malipo ya mafao, lakini pia kuna mashaka juu ya tukio hilo kulenga kuchelewesha mabadiliko ya kisiasa nchini humo.

Kiongozi mwandamizi wa baraza huru linaloongoza Sudan kwa sasa, Jenerali Mohammed Hamdan Dagalo, amemtuhumu mkuu wa zamani wa usalama wa taifa Salah Gosh kuwa yupo nyuma ya uasi huo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post