Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Kamati ya kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa mitaji ya umma [PIC] imeitaka benki ya NMB kuangalia uwezekano wa kuongeza gawio kwa serikali hali itakayosaidia kuongeza mapato katika kuchangia mfuko mkuu wa Serikali.
Akizungumza bungeni jijini Dodoma Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa mitaji ya umma [PIC] Dkt Raphael Chengeni amesema hatua hiyo itafanikisha katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo hapa nchini.
Katika hatua nyingine Dkt Chengeni amemuagiza mwenyekiti wa bodi ya benki ya NMB Profesa Joseph Semboja kuhakikisha anapeleka mbele ya kamati hiyo mchakato mzima wa kumpata mtendaji mkuu wa benki hiyo ili kutoa fursa kwa watanzania wenye uwezo na weledi wa kuongoza taasisi kubwa za kifedha wanajitokeza kwa ajili ya maslahi mapana ya taifa .
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB Bi Ruth Zaipuna amesema benki yake inaunga mkono miradi mikubwa ya kimkakati ya serikali ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) ili kurahisisha shughuli mbalimbali za kimaendeleo kwa mwananchi mmoja mmoja .
Kamati mbalimbali za bunge zinaendelea na vikao vyake jijini dodoma tangu Januari 13,2020 huku kikao cha 18 cha Bunge kikitarajia kuanza Januari ,28,2020.
Social Plugin