Jeshi la Polisi limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 33 waliohusika kwa namna moja au nyingine katika kuhusika na mauaji ya mfanyabiashara Petro Sagalika yaliyotokea siku ya tarehe 02, Januari mwaka huu katika kijiji cha Msambala wilayani Kasulu Mkoani Kigoma.
Aidha Kamishna CP Sabas amesema Mzee Perto Sagalika alikuwa Mfanyabiashara wilayani Kasulu aliekuwa anamiliki vibanda sita vya biashara, watu hao walimfuata mida ya saa kumi na mbili jioni katika eneo lake la Biashara na kuanza kumkata kata kwa mapanga mpaka kupelekea umauti wake, wakati wananchi hao wakiendelea na adhima hiyo kijana wa Mzee huyo aliweza kupata taarifa kuwa baba yake kavamiwa alifika ili kuja kumsaidia ila nae aliuliwa pia kwa kukatwa katwa kwa Mapanga.
Baada ya hatua hiyo wananchi hao wenye hasira kali walielekea nyumbani kwa Mzee Petro Sagalika na walimkuta mkewe na mwanae wa kike wakiwa wamekaa na ndipo walijichukulia sheria mkononi tena kwa kuwaua kwa kuwakata kata na mapanga mpaka kusababisha vifo vya familia nzima ya Mzee huyo baada ya kuhakikisha wameisha ua familia nzima ndipo walichukua uamuzi wa kubomoa nyumba na vibanda vyote sita vya mfanyabiashara huyo na kisha kutoweka.
Taarifa hiyo imetolewa na Kamishna wa Operesheni na Mafunzo CP Liberatus Sabas, huku akisisitiza kuwa kwavile tukio lilitokea mchana hakuna atakaesalimika kwani wahusika wote watakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria huku akiongezea mpaka sasa wamepatikana watuhumiwa 33 ila bado Operesheni inaendelea kwani hakuna jiwe litasalia juu ya jiwe.
Cp Sabas, amewataka wananchi kutoa ushirikiano katika Vyombo vya Ulinzi na Usalama huku akiwataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mikononi kwani ni kinyumea cha taratibu na sheria za nchi.