Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KANGI LUGOLA KUHOJIWA NA TAKUKURU KESHO


Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola anatarajiwa kuhojiwa kesho na Taasisi ya Kuzuia Na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo, Brigedia Jenerali, John Mbungo amesema walianza kukusanya taarifa za awali ambazo zimeshakamilika na wahusika wote wataitwa kesho kuhojiwa.

Rais Dkt John Magufuli alitengua uwaziri wa Lugola kutokana na tuhuma za utiaji saini makubaliano ya zabuni ya kununua vifaa vya Zimamoto na Uokoaji vyenye thamani ya Euro Mil. 408.2 kutoka kampuni moja ya nje ya nchi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com