Picha haihusiani na habari hapa chini
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Askari polisi aitwaye Kazimir (28) mkazi wa Shinyanga Mjini amenusurika kifo baada ya sehemu zake za siri kukatwa na kitu chenye ncha kali akiwa amelala na mkewe Flora Adam (23) kutokana na kile kinachodaiwa ni wivu wa mapenzi 'mme kuwa na mchepuko'.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga Deborah Magiligimba amesema tukio hilo limetokea Desemba 28,2019 majira ya saa 6 na nusu usiku wakati wamelala ambapo ghafla alikatwa na kitu chenye ncha kali katika sehemu ya uume wake.
“Wakiwa wamelala mke wake Frola Adam aliamka na kunyatia na kuchukua kitu chenye ncha kali na kumkata mmewe kwenye sehemu zake za siri na kumjeruhi vibaya na kumsababishia maumivu makali”,amesema Kamanda Magiligimba.
“Baada ya tukio hilo Pc Kazimir alikimbizwa katika Hospitali ya rufaa ya Serikali ya Mkoa wa Shinyanga ambako alilazwa kwa siku mbili na badaye aliruhusiwa”,ameeleza.
Amesema chanzo tukio hilo kuwa ni wivu wa kimapenzi jambo linalosadikiwa kwamba mme wake alikuwa na nyumba ndogo.
“Tunamshikilia Frola Adam (23) kwa tuhuma ya kumkata mume wake sehemu za siri na baada uchunguzi kukamilika atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili”,amesema Kamanda Magiligimba.
Social Plugin