Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Singida, Mhashamu
Edward Mapunda akizindua kituo cha Hija
eneo la Sukamahela Singida.
|
Mamia
ya wananchi wakipanda jiwe kuelekea katika kituo cha Hija kwa ajili ya Hija maalum.
|
Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Singida, Mhashamu
Edward Mapunda akimnyunyizia maji ya
Baraka Mkuu wa Mkoa wa Singida kwenye misa hiyo.
|
Na John Mapepele
SINGIDA
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema
Nchimbi amesema uzinduzi wa kituo kikubwa cha kihistoria cha Hija na
Maombezi cha Bikira Maria kilijengwa
eneo la Sukamahela ambalo ndiyo
eneo la katikati ya nchi ya Tanzania kijiografia wilayani Manyoni mkoani Singida utabadilisha
uchumi na kuchochea maendeleo ya wananchi katika kipindi kifupi kijacho
endapo wananchi watachangamkia fursa za uwekezaji katika eneo hili.
Dkt. Nchimbi ametoa rai hiyo leo
kwenye mkutano na watumishi wa umma
ambapo amesema uzinduzi wa kituo hicho
unaifanya nchi yetu kuongeza
idadi ya vivutio vya utalii wa imani
ambavyo havikuwepo kabisa hapa
nchini hivyo kuvutia wageni kutoka ndani na nje ya nchi wanaokuja kutembelea
vivutio mbalimbali kujumuisha eneo hilo.
Amewataka kwa
wananchi Mkoa wa Singida na watanzania
kufanya uwekezaji katika eneo hilo kwenye sekta za utoaji wa huduma ili kunufaika na wageni wanafika kujihi kutoka
sehemu mbalimbali duniani na kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri wa
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli za kuwaletea
maendeleo watanzania.
“Uzinduzi wa kituo cha Hija cha Bikira Maria
siyo tu kwamba utabadilisha kabisa
uchumi wa watu wetu bali utasaidia nchi yetu kukuza amani ambayo ni mhimili
mkuu wa maendeleo ya taifa lolote duniani” aliongeza dk. Nchimbi
Wakati huo huo Kanisa Katoliki nchini limetoa
pongezi na shukrani mahususi kwa Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema
Nchimbi kwa kuwa na maono ya kiroho ya kubuni wazo la kuwa na kituo hicho na
kuliwasilisha kwa kanisa
katoliki hatimaye kujengwa na kuzinduliwa kituo hicho katikati ya nchi
ya Tanzania.
Akizindua kituo hicho Januari Mosi,
Mwaka huu katika ibada maalum iliyofanyika eneo la Sukamahela, Askofu
wa Kanisa Katoliki Jimbo la Singida, Mhashamu Edward Mapunda kwa
niaba ya Kanisa Katoliki nchini alishukuru na kupongeza wazo la Mkuu wa Mkoa
wa Singida Dk. Rehema Nchimbi ambapo pia alihimiza watanzania kutumia mwaka huu
kwa sala na maombi wakati Taifa likielekea kwenye uchaguzi mkuu wa Rais,
Wabunge na Madiwani, huku akiwasihi Wakristo nchini kote kumtumia Mama Bikira
Maria ili aweke uchaguzi huo kwenye Moyo wake mtakatifu kwa sababu yeye ni
Malkia wa Amani.
Maria alikuwa mwanamke Myahudi aliyeishi kati ya karne ya 1 KK
na karne ya 1
BK. Mke wa Yosefu, alimzaa Yesu Kristo.
Kwa sababu hiyo na kwa utakatifu wake anapewa heshima ya pekee katika madhehebu
mengi ya Ukristo,
lakini pia katika Uislamu duniani kote.
Wakiongea kwa nyakati tofauti siku ya uzinduzi wa kituo hicho wananchi wa Sukamahela
walisifu na kupongeza ubunifu wa Mkuu
wa Mkoa katika mambo mbalimbali katika
taifa letu.
“Ndugu yangu
kwa kusema ukweli tunamshukuru sana mungu kwa
kumpa Mkuu wetu wa Mkoa wa
Singida mama Nchimbi maono yanayoleta mapinduzi ya kiroho, kiuchumi na kijamii
maana amefanya mapinduzi makubwa pia katika kilimo cha Korosho”alilisitiza Eliakimu
Joseph ambaye ni mkazi wa Manyoni
Naye Jummanne Mwenda mkazi wa Singida mjini amesema kuwa mageuzi
kama ya korosho aliyafanya Dkt. Nchimbi akiwa mkoani Njombe ambapo alihamasisha
kilimo cha parachichi ambacho wananchi wa mkoa huo wameendelea kunufaika nacho hadi
sasa.
Social Plugin