Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), James Kilaba amesema uzimaji wa laini za simu ambazo hazijasajiliwa kwa alama za vidole unafanyika kwa Awamu.
Amesema zoezi hilo lililoanza jana Januari 20, 2020 linafanyika kwa Awamu ili kuondoa usumbufu na hadi kufikia jana usiku saa nne walikuwa wamezima laini 975,041
Amesema, kundi la kwanza waliozimiwa laini ni watu 656,091 ambao wana Vitambulisho vya Taifa au Namba lakini hawajasajili laini zao
Amebaisha kuwa, kundi la pili ni watu 318,950 waliosajili laini zao kwa Kitambulisho cha Taifa kabla ya kuanza mfumo wa kusajili kwa Alama za Vidole
Amesema, “Tunazima kidogo kwa sababu ya mambo ya kitaalamu, hauwezi ukazima laini milioni tano au 10 kwa mara moja kwa maana watajazana kwenye kusajili kitu kinachofanya Mifumo ya NIDA inaelemewa"
Social Plugin