Maelfu ya waombolezaji wamekusanyika leo Jumamosi mjini Baghdad kushiriki maandamano ya mazishi ya kamanda wa jeshi la Iran Qasem Soleimani, aliyeuawa katika shambulio la angani lililotekelezwa na Marekani siku ya Ijumaa.
Wengi wa waombolezaji walivalia nguo nyeusi na kubeba bendera za Iraq pamoja na bendera za wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran ambao ni watiifu kwa jenerali Soleimani.
Soleimani alikuwa kiungo muhimu katika oparesheni ya Iran Mashariki ya kati na taifa hilo limeapa "kulipiza kisasi" mauaji yake.
Waandamanaji walianza kukusanyika mjini Baghdad mapema asubuhi ya Jumamosi wakipeperusha bendera ya Iraq naya waasi wakiimba "kifo kwa Amerika".
Waandamanaji walizunguka barabara za mji huo wakibeba mababgu yaliyo na picha ya Soleimani huku wengine wakiwa na mabangu yaliyo na picha ya kiongozi mkuu wa kidini wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei.
Ripoti zinasema mwili ya raia huyo wa Iran aliyeuawa katika shambulio hilo utasafirishwa nchini humo Jumamosi jioni, ambako siku tatu ya maombolezo imetangazwa kwa heshima ya jenerali.
Mazishi yake yatafanyika siku ya Jumanne nyumbani kwake Kerman eneo la kati la Iran.
Social Plugin