Mahakama ya Kisutu imetupilia mbali ombi la Erick Kabendera kwenda kutoa heshima za mwisho kufuatia kifo cha mama yake mzazi.
Hakimu Janeth Mtega amesema mahakama haina mamlaka ya kutoa ruhusa hiyo, na mtuhumiwa hana fursa ya kukata rufaa kupinga uamuzi huo.
Maombi hayo yaliwasilishwa na mawakili wake wakiongozwa na Jebra Kambole.
Kwa upande wake Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alitoa pole kwa Erick kufiwa na mama yake ambapo licha ya pole hizo, upande wa mashtaka ulipinga ombi hilo kwa madai ya kuwa hoja za upande wa utetezi hazikuwa na mashiko.
Kesi imeahirishwa hadi Januari 13.
Mwili wa Verdiana Mujwahunzi (80), mama mzazi wa mwandishi wa habari nchini Tanzania, Erick Kabendera aliyefariki dunia Desemba 31, 2019 katika Hospitali ya Rufaa Amana jijini Dar es Salaam utagwa kesho Ijumaa Januari 3, 2019 Chang’ombe Dar es Salaam kisha kusafirishwa kwenda Bukoba mkoani Kagera kwa maziko yatakayofanyika Januari 6, 2020.
Social Plugin