Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo la mvua kubwa kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe, Iringa, Ruvuma, Lindi, Mtwara pamoja na kusini mwa mkoa wa Morogoro.
Taarifa iliyotolewa leo Ijumaa Januari 31, 2020 na TMA imesema athari zinazoweza kujitokeza ni baadhi ya makazi kuzungukwa na maji, ucheleweshwaji wa usafiri, kusimama kwa muda kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi na kijamii.
Kesho Jumamosi Februari 1, 2020 TMA imetoa tahadhari ya mvua kubwa kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Ruvuma, Njombe, Iringa, Songwe, Mbeya, Singida, Dodoma pamoja na kusini mwa mkoa wa Morogoro.
“Angalizo la mvua kubwa kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Lindi, Mtwara, Manyara, Kilimanjaro, Arusha, Shinyanga, Simiyu, Mwanza, Mara, kaskazini mwa mkoa wa Morogoro, Pwani, Dar es Salaam, Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba,” imesema taarifa hiyo
Jumapili ya Februari 2, 2020 TMA imetoa angalizo la mvua kubwa kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Ruvuma, Njombe, Iringa, Songwe, Mbeya, Singida, Morogoro, Lindi, Mtwara, Manyara, Kilimanjaro, Arusha, Shinyanga, Simiyu, Mwanza na Mara.
Social Plugin