MAREKANI YAKIRI WANAJESHI WAKE 11 WALIJERUHIWA NA MAKOMBORA YA IRAN


Licha ya Marekani  hapo awali kudai kuwa hakuna askari wake  aliyeuawa au kujeruhiwa katika mashambulizi 22 ya Makombora ya  Iran dhidi ya kambi mbili za kijeshi za nchi hiyo huko Iraq, lakini hivi sasa imefichuka kuwa, wanajeshi kadhaa wa Marekani  walijeruhiwa vibaya na wakupelekwa kwa usafiri wa ndege katika nchi za Ujerumani na Kuwait kwa ajili ya matibabu.

Hapo jana, maafisa wa Marekani walilazimika kukiri juu ya kujeruhiwa wanajeshi wa nchi hiyo na makombora ya Iran, licha ya hapo awali kukataa  kuwa kulikuwepo na majeruhi katika shambulizi hilo

Masaa machache baada ya Iran kuvurumisha makombora na kupiga kambi mbili za Marekani nchini Iraq, Rais Donald Trump alijitokeza na kudai kuwa, "Ni furaha kuwatangazia Wamarekani kuwa hakuna askari wetu hata mmoja aliyeuawa au kujeruhiwa katika shambulizi la makombora la Iran nchini Iraq."


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post