MCHUNGAJI mmoja nchini Kenya amemuua mkewe, Ann Mghoi, kwa kumchoma visu, kisha na yeye kujiua.
Mchungaji huyo aliyefahamika kwa jina la Elisha Misiko alimuua mkewe ndani ya kanisa lake lililopo katika kijiji cha Chembani, Kisauni, Mombasa na baadaye kujikata koo hadi kufa.
Misiko aliyekuwa mchungaji wa kanisa la Goods for God’s Gospel Ministries ameacha ujumbe unaomlaumu mkewe kwa kuwa na mahusiano na kijana mdogo katika kanisa hilo, lakini pia katika ujumbe huo amemlaumu mkewe kwa kumzuia kuwaona watoto wao.
Mmoja wa polisi wa Kisauni, Julius Kiragu, ameeleza kuwa mchungaji huyo ameacha makaratasi 17 yaliyoandikwa kama wosia wake akibainisha sababu za kuchukua maamuzi hayo.
Social Plugin