Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahuu ameikatiza ziara yake ya Ugiriki kufuatia kuuawa kwa Meja Jenerali Qassem Soleimani, mkuu wa jeshi maalum la Iran.
Hayo ni kwa mujibu wa afisa mmoja kutoka ofisi ya Waziri Mkuu huyo.
Netanyahu amekuwa mjini Athens kufuatia muafaka uliotiwa saini na Ugiriki, Cyprus na Israel hapo jana, wa kujenga bomba la kusafirisha gesi asili kutoka eneo linakopatikana mafuta la mashariki ya Mediterania hadi Ulaya.
Redio ya Jeshi la Israel imeripoti kuwa jeshi la nchi hiyo liko katika hali ya tahadhari kubwa, likihofia ulipizaji kisasi wa Iran au washirika wake baada ya kuuliwa kwa Soleimani katika shambulizi la angani mjini Baghdad.
Wakati huo huo, Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Marekani imewataka raia wa Marekani kuondoka nchini Iraq haraka iwezekanavyo.
Shughuli za ubalozi wa Marekani mjini Baghdad zilisitishwa mapema wiki hii kufuatia mashambulizi kwenye jengo la ubalozi na wafuasi wa wanamgambo wanaoungwa mkono na Iraq.
#Iraq: Due to heightened tensions in Iraq and the region, we urge U.S. citizens to depart Iraq immediately. Due to Iranian-backed militia attacks at the U.S. Embassy compound, all consular operations are suspended. U.S. citizens should not approach the Embassy. pic.twitter.com/rdRce3Qr4a— Travel - State Dept (@TravelGov) January 3, 2020
Waziri mkuu wa Iraq anaeondoka Adel Abdul-Mahdi amelaani mashambulizi ya Marekani na kuitishia kikako cha dharura cha Bunge kuchukuwa kile alichokiita hatua stahiki zinazohitajika ili kulinda hadhi, mamlaka na uhuru wa Iraq.
Mataifa mengine pia yamezungumzia mauaji hayo ambapo Urusi imesema yanaweza kuchochea zaidi mzozo katika kanda ya Mashariki ya Kati, huku Ufaransa ikisema mauaji ya Soleimani hayatatuliza mzozo bali yatauchochea zaidi.
China kwa upande wake imeomba pande zote kujizuia huku utawala wa Syria ukilaani pia mauaji hayo uliyoyataja kama ya kiuoga kwa upande wa Marekani.
Social Plugin