Na Amiri Kilagalila-Njombe
Jeshi la polisi mkoani Njombe linamshikilia ndugu Josphat Mtega (24) mkazi wa Ramadhani mjini Njombe kwa tuhuma za kumsababishia kifo mkewe kilichotokana na ugomvi.
Akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake,kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa amesema mtuhumiwa huyo anashikiliwa na jeshi la polisi kutokana na kugombana na mkewe Angelina Sanga (24) ambapo inadaiwa alimpiga na hivyo kumsababishia majeraha makubwa yaliyosababisha kifo chake.
Kamanda amesema mara baada ya ugomvi huo, Angelina alisafirishwa hadi hospitali ya Ikonda iliyopo wilayani Makete ambapo baada ya kufikishwa katika hospitali hiyo uchunguzi wa kitabibu ulibaini kuwa dada huyo alionekana amevunjika mkono na sehemu mbali mbali za mwili wake zilionekana zimeshambuliwa vibaya.
Amesema mwanaume huyo anaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi huku taratibu za kisheria zikiendelea.
Social Plugin