Na Amiri Kilagalila-Njombe
Mzee Jonaidi Haule (72) mkazi wa Mawengi wilayani Ludewa Mkoani Njombe amesababishiwa kifo kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali na mwanae kutokana na ugomvi wa kifamilia.
Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa amesema baada ya ugomvi kuibuka na kusababisha hali ya kuto kuelewana kati ya mtoto na baba yake, ,mtoto aliyefahamika kwa jina la Jailos Thomas Haule alichukua kitu chenye ncha kali na kumjeruhi baba yake.
Kamanda amesema mara baada ya kujeruhiwa mzee huyo alifikishwa katika matibabu hospitali ya wilaya ya Ludewa na kupoteza maisha mara baada ya hali yake kuwa mbaya zaidi.
Aidha kamanda wa polisi amesema jeshi hilo linamtafuta mtuhumiwa Jailos Haule aliyetokomea kusikojulikana kwa tuhuma za kesi ya mauaji.
Social Plugin