Benedictor Gogogo (48) mkazi wa Itabagumba, Sengerema mkoani MWANZA amechanwa tumbo na kitu chenye ncha kali hadi utumbo kutoka nje baada ya kutokea ugomvi kati yake na mke wake
Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Jumanne Murilo amesema tukio hilo lilitokea jana na wanamashikilia Mtuhumiwa kwa mahojiano na uchunguzi zaidi
Akiwa hospitalini, Gogogo amesema mzozo kati yake na mke wake aliyemtaja kwa jina la Mama Asteria ulitokana na kuhoji matumizi ya Tsh. 10,000 aliyoacha nyumbani asubuhi ya siku hiyo
Amesema, “Wakati naondoka kwenda kwenye shughuli zangu za uvuvi, asubuhi ya siku ya tukio, niliacha Tsh. 10,000 ya matumizi. Niliporejea nilimwomba anipe Tsh. 1,000 ninunulie vocha ya simu lakini akaniambia fedha yote imeshatumika.”
Ameongeza, “Nilipohoji zaidi akaanza kunitolea majibu yaliyonikasirisha na kunifanya nimpige kofi na kutokea mzozo kati yetu ambao hata hivyo uliisha na mimi kuingia ndani kujipumzisha.”
Aidha, Gogogo ameeleza kuwa akiwa ameanza kupitiwa usingizi, mke wake ambaye wameishi mwaka mmoja na nusu sasa alimvizia na kumchana na kitu chenye ncha kali tumboni hadi utumbo kutoka nje
Social Plugin