Na Amiri Kilagalila-Njombe
Naibu waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dkt.Faustine Ndungulile amemzuia mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa,mganga mkuu wa wilaya, pamoja na timu ya wasimamizi wa huduma za afya kusafiri ndani ya miezi miwili mpaka utakapobadilishwa mfumo mzima wa uendeshaji wa huduma za afya wilayani humo.
Dkt.Ndungulile ametoa agizo hilo wilayani Ludewa mkoani Njombe mara baada ya kukagua shughuli za vikundi mbali mbali,na mwenendo wa utoaji wa huduma za afya katika wilaya hiyo na kubaini mapungu makubwa katika uendeshaji wa huduma za afya za wilaya.
“Nimewapeni miezi miwili ya kufanya marekebisho makubwa,ndani ya mfumo mzima wa uendeshaji wa huduma za afya Ludewa,na nimeshatoa maelekezo Mkurugenzi,DMO na CHMT yake hakuna kusafiri kwa muda wa miezi miwili”aliagiza Dkt.Ndungulile
Amewata kukaa katika wilaya hiyo na kutembelea vituo vyote vya afya na kuweka mifumo mizuri ya usimamizi huku kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo pia ikitakiwa kukagua utoaji wa huduma.
Social Plugin