MWANDISHI WETU Lagos, Nigeria
BENKI ya United ya Afrika Plc (UBA), imetangaza safu mpya ya uongozi
huku Oliver Alawuba, akiteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa UBA Africa,
anayesimamia shughuli za nchi 20 za Afrika akitoa Nigeria.
Hatua hiyo inatokana na baadhi ya viongozi wake kustaafu katika bodi
akiwamo Victor Osadolor, ambaye alitumikia nafasi hiyo kwa miaka tisa.
UBA for Africa inahudumia wateja zaidi ya milioni 19 katika Bara la
Afrika, ikitoa huduma za rejareja, biashara na taasisi za kitaifa na
inaongoza katika huduma jumuishi za kifedha na utekelezaji wa miradi
katika nchi za Afrika.
Taarifa iliyotolewa na benki hiyo jana, ilieleza kuwa UBA inatajwa kuwa
ni moja ya benki iliyowasiliana na mteja moja kwa moja kupitia chatbot
iitwayo LEO.
Alawuba ana miongo mitatu ya uzoefu katika tasnia ya benki. Ambapo pia
aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa UBA Ghana na baadaye kuwa Mkurugenzi
Mtendaji UBA Africa kabla ya kurudi Nigeria kuendesha Benki ya UBA ya
ukanda wa mashariki.
Chini ya uongozi wake, Benki ya UBA ya ukanda wa Mashariki imekuwa ni benki inayokua kwa kasi zaidi katika Afrika.
“Pia Bodi ilimteua msenegali, Abdoul-Aziz Dia kama Mkurugenzi Mtendaji
wa Hazina na huduma ya benki Kimataifa, kwa idhini ya Benki Kuu ya
Nigeria.
Aziz anakuwa mkurugenzi mtendaji na atasaidia kwa zuoefu wake
aliopitia nchi mbalimbali kukuza maendeleo ya benki ya UBA.
“Dia atawajibika kwa mtandao wa kimataifa wa shughuli za UBA huko New
York, London na Paris, pamoja na Hazina kwa ujumla, ambapo UBA inatoa
sehemu kubwa ya bidhaa kwa mataifa, taasisi za kimataifa na wateja wa
Afrika,” ilieleza taarifa hiyo.
Mbali na hao pia Chukwuma Nweke, ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa
huduma za rejareja na malipo, ambapo ameonyesha dhamira yake kwenye
taasisi kwa upande wa huduma za kibenki za rejareja.
Chukwuma ana karibu miongo mitatu ya uzoefu wa benki unaochukua Operesheni za Benki, Fedha, Teknolojia, ukaguzi na mkakati.
Bodi pia ilitangaza uteuzi wa Chiugo Ndubisi kama Mkurugenzi mkuu na
mkuu wa uendeshaji wa UBA kwa idhini ya Benki Kuu ya Nigeria.
Akizungumzia kuhusu uteuzi huo, Mwenyekiti wa UBA, Tony O. Elumelu
alisema “Miadi hii inasisitiza kujitolea kwa UBA kwa mtandao wetu wa
Afrika na wa ulimwengu, msingi wetu mkubwa wa wateja na miundombinu yetu
ya utendaji.
Tunaangazia kuboresha ufanisi wetu na kuimarisha zaidi
utumishi wetu kwa Afrika, kwa kutumia vipaji vya ajabu na uzoefu
unaopatikana katika taasisi yetu,” alisema
Elumelu amewashukuru Mkurugenzi Msaidizi / Mkurugenzi Mtendaji
anayemaliza muda wake wa uongozi wa UBA Afrika, Victor Osadolor na
Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa UBA kanda ya Mashariki na Kusini mwa
Afrika, Emeke Iweriebor, ambaye amestaafu katika bodi, kwa michango yao
mikubwa waliotoa kwa Benki ya UBA.
“Victor na Emeke walikuwa watu muhimu wakati wa kuunganishwa kwa Benki
ya Standard Trust na UBA na wamekuwa wachangiaji muhimu katika ukuaji wa
Benki. Tunawatakia maisha mema,” alisema Tony.
Uteuzi mpya wa Bodi umezingatia uwekezaji mkubwa katika rasilimali watu
kwa kuchagua watendaji wenye sifa stahiki na utendaji mkubwa kaika
kuendeleza benki.
Benki ya UBA imeweza kukaribisha wafanyakazi wapya 3000 kwa mwaka 2019,
na kuwaongeza vyeo Zaidi ya wafanyakazi 5000. UBA ni muajiri mkubwa
katika sekta ya benki Nigeria ikiwa na waajiriwa Zaidi ya 20,000 kwa
grupu nzima.
Social Plugin