Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAALIM SEIF NA SALIM BIMANI WATUHUMIWA KUFANYA MKUTANO BILA KIBALI


Mshauri Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad na Mwenyekiti wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho, Salim Bimani wametuhumiwa kufanya Mkutano bila kibali mnamo Desemba 2019, huko Micheweni Zanzibar.

Hata hivyo, Viongozi hao wameachiwa kwa dhamana na Chama chao kupitia Mtandao wa Twitter kimedai walifanya Mkutano wa ndani usiohitaji kibali

Viongozi hao waliripoti Polisi asubuhi ya leo kuitikia wito wa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (RCO) wa Mkoa wa Kaskazini Pemba


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com