Aliyekuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye akiingia Makao Makuu ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) jijini Dodoma, kwa ajili ya mahojiano.
Andengenye anakuwa kiongozi wa tatu kuhojiwa kuhusiana na sakata la viongozi chini ya wizara hiyo, kusaini makubaliano ya zabuni ya kununua vifaa vya zimamoto na uokoaji vyenye thamani ya Euri 408 (sawa na Sh trilioni moja) kutoka kampuni moja nje ya nchi bila kufuata sheria.
Wengine ni aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu.