Mbunge wa Mwibara(CCM) Kangi Lugola akiwa Bungeni hii leo jijini Dodoma akihudhuria vikao vya Bunge huku akitumia 'ipad kusoma na kutafakari kikao cha pili cha Mkutano 18 wa Bunge.
Kangi alikuwa Waziri wa mambo ya ndani ambaye uteuzi wake ulitenguliwa juma liliopita.
Lugola aliondolewa Uwaziri baada ya kuhusishwa na kashfa ya Mkataba wa Tsh. Trilioni 1 wa ununuzi wa vifaa vya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brig. Jen. John Mbungo amesema, uchunguzi huo umeanza kama sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Rais Magufuli aliyekabidhi suala hilo kwao kwa hatua zaidi na kuisihi Mamlaka hiyo kutowaonea huruma waliohusika
Social Plugin