Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha: MASPIKA WASTAAFU WA BUNGE WAKABIDHIWA MAJOHO YAO WALIYOKUWA WAKIYATUMIA

Bunge la Tanzania limeamua kuwapa heshima maspika wastaafu kwa kuwakabidhi majoho waliyokuwa wakiyatumia.


Shughuli hiyo ya kukabidhi majoho imefanyika leo katika kikao cha kwanza cha mkutano wa 18 wa Bunge.

Joho la Spika wa Bunge la tisa marehemu Samuel Sitta limepokelewa na mkewe Margaret Sitta ambaye ni mbunge wa Urambo (CCM).

Margaret ameungana na maspika wastaafu, Pius Msekwa na Anne Makinda kupokea majoho waliyoyatumia wakati wakiongoza chombo hicho cha Dola kwa nyakati tofauti.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com