RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akikagua gwaride Maalum la Maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza vla Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwasalimia Wananchi wakati wa Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar
Mgeni rasmi,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar wa awamu ya sita Dk. Amani Abeid Karume alipowasili jukwaa kuu,katika Maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar.Pichani kati anaeshuhudia ni Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete.
VIJANA wa Maandamano Maalum ya kuadhimisha Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiwa na Picha za Waasisi wa Mapinduzi, wakati wa hafla hiy0 iliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar.
Vijana wa Chama cha mapinduzi wakipita mbele ya Mgeni Rasmi ikiwa ni Ishara ya kutoa heshima katika maandamano ya maadhimisho ya ya Miaka 56 ya Mapinduzi yaliofanyika Aman mjini Zanzibar.
WANACHAMA wa Chama cha CUF wakishiriki katika Maandamano ya kuadhimisha sherehe za Miaka 56 ya Mapinduzi Zanzibar zilizofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar
VIJANA wa payunia wakitowa salamu ya heshima kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein wakati wa maandamano ya Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Vikosi vya Jeshi la Ulinzi na Usalama Vikipita mbele ya Mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akitoa hotuba ya Makaribisho kwa Mgeni Rasmi katika kilele cha Maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi yaliofanyika Aman mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein akitoa hotuba ya kilele cha Maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi yaliofanyika Aman mjini Zanzibar.
PICHA NA IKULU PAMOJA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.
Social Plugin