Baada ya kupokea taarifa ya Watu wawili kujinyonga mpaka kupoteza maisha Tabora, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Barnabas Mwakalukwa amesema Polisi wataanza msako wa kuwabaini na kuwakamata wote wanaotarajia kujinyonga mwaka huu na kuwapelekea Mahakamani.
Kwa mujibu wa RPC Mwakalukwa, walijionyonga ni Mwalimu Basil Sungu (39) wa shule ya msingi Ikongolo Wilaya ya Uyui mkoani Tabora ambaye amejinyonga hadi kufa kwa kutumia kipande cha kitenge cha mke wake.
Amesema mwili wa Sungu ulikutwa chumbani kwake ukiwa unaning’inia darini Jumanne iliyopita ya Desemba 31, 2019.
Mwingine ni James Albert (22), mjasiriamali na mkazi wa kata ya Chemchem Manispaa ya Tabora ambaye amekutwa amejinyonga hadi kufa kwa kutumia mkanda wa begi.
“Niwambie mwaka huu tabia hizo zikome kwa wanaotegemea kujinyonga tutaanzisha doria kuhakikisha wote wanaotarajia kujinyonga mwaka huu tunawakamata kabla hawajinyonga na tunawapelekea mahakamani” Amesema RPC Mwakalukwa huku akisema uchunguzi dhidi ya matukio haya mawili unaendelea ili kujua chanzo
Social Plugin