Jamaa wawili wamefikishwa mahakamani Jumanne ,Disemba 31, 2019 baada ya kukashifiwa kwa kuiba chupa sita za pombe aina ya Jameson.
Daniel Mbugua na Cliff Obonyo ambao ni wafanyakazi wa kampuni ya Mitchel Cot wanasemekana kutekeleza kitendo hicho Disemba 17, wakiwa mtaani Embakasi.
Pombe hiyo ni ya thamani ya KSh 15,000.
Washukiwa hao wanasemekana kuficha pombe hiyo kwenye gari la kampuni ambalo husafirisha mizigo na bidhaa.
Wawili hao walikana mashtaka dhidi yao na kuachiliwa kwa dhamana ya KSh 20,000 kila mmoja. Kesi dhidi yao itasikizwa tena Aprili 28, 2020.
Social Plugin