Wafanyakazi watatu wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani wameuawa kwenye shambulizi la kigaidi katika kambi ya kijeshi ya Manda ilioko mjini Lamu.
Wafanyakazi 2 pamoja na makandarasi wawili wameripotiwa kuachwa na majeraha mabaya kufuatia shambulizi hilo la Jumapili, Januari 5.
" Wakati wa shambulizi hilo la kigaidi katika kambi ya kijeshi ya Manda, wafanyakazi wa wizara ya ulinzi ya Marekani waliuawa, huku wengine wawili wakijeruhiwa vibaya ila hawako katika hali mbaya,"Sehemu ya taarifa ya ubalozi wa Marekani ilisoma.
Aidha, Marekani imeapa kupambana vilivyo na magaidi wa al- Shabaab hasa wale waliotekeleza shambulizi la Manda.
Social Plugin