Rais Magufuli amesema Serikali imejipanga kuhakikisha uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba, 2020 unakuwa wa amani, uhuru na haki.
Amesema utakapofika uchaguzi huo, nchi na taasisi mbalimbali zitakaribishwa Tanzania kushuhudia.
Ametoa kauli hiyo jana Jumanne Januari 21, 2020 alipokutana na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania katika sherehe za mwaka mpya 2020 na chakula cha jioni zilizofanyika Ikulu, Dar es Salaam.
Amebainisha kuwa uchaguzi ni jambo muhimu, Serikali imejipanga kuandaa mazingira mazuri katika uchaguzi huo.
“Oktoba mwaka huu wa 2020 nchi yetu itafanya uchaguzi mkuu, zoezi la uchaguzi ni muhimu kwa nchi yoyote inayofuata misingi demokrasia, Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa uchaguzi mkuu unafanyika katika mazingira ya amani, uhuru na haki,” amesema Rais Magufuli.
Amesema ukikaribia uchaguzi huo nchi mbalimbali na taasisi za zitakaribishwa Tanzania kushuhudia
“Kama ilivyo kawaida yetu wakati ukifika tutazikaribisha nchi na taasisi mbalimbali kuja kuangalia uchaguzi wetu ili kujionea jinsi nchi yetu inavyokomaa katika nyanja ya demokrasia,” amesema Magufuli
Social Plugin