Kamanda wa Polisi Temeke, Amon Kakwale, amesema chanzo cha moto uliotokea usiku wa kuamkia leo katika matanki ya mafuta ya kampuni ya Lake Oil, eneo la Kigamboni, umesababishwa na hitilafu ya mota inayosukuma mafuta kutoka chini na kupandisha juu, iliyopelekea cheche na kuleta mlipuko.
Kamanda Kakwale amesema licha ya kufanikiwa kuuzima moto huo, Askari mmoja wa Jeshi la Zimamoto alipata mshituko baada ya kuingia kwenye chemba moto ulikoanzia na kuuzima.
"Mota ilipata hitilafu za kiufundi ambayo ilizalisha cheche za moto kutoka kwenye chemba ndogo ya chini, madhara yaliyotokea ni mwenzetu wa uokoaji mmoja, moshi ulimuingia kwenye kinywa na kupata mshituko kidogo" amesema Kamanda Kakwale.
Aidha Kamanda Kakwale ameongeza kuwa hadi sasa bado uongozi wa kampuni ya mafuta ya Lake Oil, haijawapelekea ripoti kamili inayoonesha ni athari kiasi gani imetokea.
Social Plugin