Mzee Zacharia Ndemfoo (83) enzi za uhai wake (picha ya mwaka 2008).
Gwiji na Mkongwe wa salamu Redioni Mzee Zacharia Ndemfoo (83) wa Machame Kisiki Moshi mkoani Kilimanjaro amefariki dunia jana Ijumaa Januari 17,2020.
Kupitia mtandao wa Facebook Mtuma Salamu Fikiri Dario Gakala ameandika ujumbe ufuatao.
Imethibitika Gwiji na Mkongwe wa salamu mzee Zacharia Ndemfoo amefariki Dunia hapo jana,
Mzee Ndemfoo wa Machame Kisiki Moshi nimeanza kumsikia tangu mwaka 1994 Dw,lakini yeye mwenyewe aliwahi kuniambia ameanza kutuma salamu Dw 1965, pia aliniambia yeye alizaliwa 1937,
Picha hiyo niya 2008 Kazi ya Mungu haina makosa,mbele yetu nyuma yake.
Social Plugin