SHULE 10 JIJINI TANGA ZANUFAIKA NA MSAADA WA KOMPYUTA ZILIZOTOLEWA NA MBUNGE UMMY MWALIMU



 Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kulia akigawa msaada wa moja ya kumpyuta 20 kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari kulia leo ambapo shule 10 zitanufaika na msaada huo ambao umetolewa Mbunge huyu kwa ufadhili wa  Tume ya Mawasiliano nchini wenye thamani ya milioni 16.

 Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kulia akigawa msaada wa moja ya kumpyuta 20 kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Mnyanjani Saida Mahadhi kushoto jana ambapo shule 10 zitanufaika na msaada huo ambao umetolewa Mbunge huyo kwa ufadhiliwa na Tume ya Mawasiliano nchini wenye thamani ya milioni 16 kulia  ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Msaafu wa Jeshi Mkoba

 Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kulia akigawa msaada wa moja ya kumpyuta 20 kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari kulia leo ambapo shule 10 zitanufaika na msaada huo umetolewa na Mbunge Ummy kwa ufadhili wa  Tume ya Mawasiliano nchini wenye thamani ya milioni 16 katikati mwenye miwani ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji na kushoto Mwenye Kaunda suti ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa

 MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa halfa ya makabidhiano hayo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa


 Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa halfa hiyo kushoto ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na kulia ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji

Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji akizungumza wakati wa makabidhiano hayo

 Afisa Elimu Jiji la Tanga Lusajo Gwakisa akitoa taarifa ya elimu wakati wa makabidhiano hayo

 Sehemu ya wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo walimu wakuu wa shule za sekondari na wadau wakifuatilia makabidhiano hayo

Sehemu ya walimu wa shule ya Sekondari Mkwakwani wakifuatilia makabidhiano hayo


 Sehemu ya Kompyuta zilizotolewa na Waziri Ummy kwa shule 20 za sekondari Jijini Tanga

 Sehemu ya Kompyuta zilizotolewa na Waziri Ummy kwa shule 20 za sekondari Jijini Tanga 


SHULE 10 za sekondari Jijini Tanga zimenufaika na msaada wa Kompyuta 20 ambao zimetolewa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Ummy Mwalimu. 


Msaada huo ambao umetolewa na Mbunge Ummy ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto kwa ufadhili wa Tume ya Mawasiliano nchini wenye thamani ya sh.milioni 16.


Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo yaliyofanyika kwenye shule ya Sekondari Mkwakwani, Mbunge Ummy alisema kwamba uwepo wa kompyuta hizo utatoa fursa kwa wanafunzi kusoma somo hilo kwa vitendo ikiwemo kusaidia utendaji wa kazi wao.


Alisema piaa ametoa kompyuta hizo kwa shule hizo ili kuwasaidia wanafunzi kujifunza somo  na kurahisisha bajeti za shule ngazi ya shule na uandaaji wa malipo kwa kutumia mfumo wa FFARS na sio watumie kucheza karata bali


“Lakini pia zitasaidia usajili wa wanafunzi na usajili wa watahiniwa vyote vitasaidia hivyo Mkurugenzi wa Jiji Daudi Mayeji wasaidia WIFI kwa lengo la kurahisisha baadhi ya mambo yanayohitajika kutumia mtandao”Alisema


 Mbunge huyo alisema kwamba kwa shule ambazo hazijapata msaada huo atakwenda kutafuta lengo lake ni kutafuta vishkwabi kwa ajili ya wanafunzi kuhakikisha wanasoma somo la kompyuta huku akihaidi pia kujengwa vyumba vitano vya madarasa


“Niwashukuru lakini niendelee kuwaomba wanafunzi fanyeni kazi kwa kujitumua na tunatambua vipi changamoto za walimu tutaendelea kuzipatia ufuimbuzi”Alisema

Hata hivyo amehaidi kwamba ataendelea kuwasemea wananchi wa Jiji la Tanga kwa kutumia nafasi yake kuhakikisha maslahi ya walimu yanakuwa mazuri.


Awali akizungumza katika makabidhiano hayo Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa alisifu juhudi zinazofanywa na Mbunge Ummy kuhakikisha anawasaidia wananchi wa Jiji la Tanga kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili kwenye sekta mbalimbali ikiwemo ya elimu.


Alimpongeza Waziri Ummy kwa msaada huo ambao amewapatia shule hizo kwani miongoni mwao ni zile ambazo zinaupungufu wa madarasa zimenufaika na msaada huo wa kompyuta.


Naye kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji alisema kwamba msaada huo wa komputa utakuwa chachu kubwa kwao kwani serikali ya sasa imefanya mageuzi makubwa.


Alisem kutokana na mageuzi hayo hakuna malipo yanayoweza kufanyika bila mfumo kwa hiyo msaada huo wa kumputa 20 shule hizo zitakuwa zimeondolewa kwenye tatizo la kutokuweza kufanya malipo kutumia mfumo.


“Kutokana na kwamba shule nyingi au Taasis zimekuwa zikienda shule za jirani kutokana wengi kutokuwa nazo hivyo msaada huo utakuwa chachu kubwa kwa kuongeza ufanisi katika utendaji wao “Alisema.


Awali akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Afisa Elimu Jiji la Tanga Lusajo Gwakisa alimshukuru Mbunge Ummy kwa msaada huo wa kompyuta 20 utakwenda kupunguza upungufu uliopo wa Kompyuta bali italeta tija katika maendeleo.


“Maendeleo hayo ambayo msaada huu utaleta tija ni utayarishaji wa bajeti katika ngazi za shule lakini pia uandaaji wa malipo kwa kutumia mfumo wa FFARE pamoja na usajili wa wanafunzi wanaoanza kidato cha kwanza “Alisema


Hata hivyo alisema kwamba pia vitasaidia uhamishaji wa taarifa za wanafunzi kwa kutumia mfumo wa PREM ikiwemo usajili wa watahiniwa wa kidato cha pili,nne na sita na kutunza kumbukumbu nyengine za utawala.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post