Baadhi ya Watanzania wamejiunga na marafiki zao wa China
kusherehekea sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa Kichina inayokaribia kwenye
tamasha kubwa la Heri ya Mwaka Mpya wa Kichina 2020.
Shughuli
hizo zimefanyika nchini Tanzania kwa miaka kumi mfululizo, ambazo zinaonesha
kukaribia kwa mwaka mpya wa jadi wa kichina.
Kwa
niaba ya Makamu wa Rais wa Tanzania Mheshimiwa Samia Hassan Suluhu, Waziri wa
nchi wa Tanzania Mheshmiwa George
Simbachawene amesema, watanzania wanafurahia kujumuika na wachina kusherehekea
mwaka mpya wa jadi, pia amesema Tanzania na China ni marafiki wakubwa.
Habari pia zinasema mamia ya
watu wa China na Afrika Kusini kutoka sekta mbalimbali jana walikusanyika
kwenye Uwanja wa Nelson Mandela huko Johannesburg na kusherehekea mwaka mpya wa
jadi wa kichina.
Wasanii wa China na Afrika
Kusini walifanya maonesho ya Kung Fu, sarakasi, opera ya Sichuan na sanaa ya
chai ya Kichina, na kuwavutia watazamaji.
Social Plugin