Benki ya TPB imetoa elimu kwa walimu wastaafu wilayani kahama kuhusu maboresho ya huduma zao lakini namna gani mzee anapaswa kuwekeza na kuwa na matumizi bora ya pesheni yake.
Akizungumza katika mkutano huo Januari 4,2020 Meneja wa Benki ya TPB mkoa wa Shinyanga Jumanne Wagana
aliwapa wazee Elimu ya BIMA ya Maisha ya Tsh 1000/=, Biashara ya akaunti ya Amana kwa muda maalumu inayokupa faida mpaka 12%, jinsi ya kupata mitaji kupitia mikopo ya riba nafuu ya wastaafu, mikopo ya kilimo, mikopo ya biashara n.k.
Katika mkutano huo ambao ulifadhiliwa na Benki ya TPB wastaafu mbalimbali walitoa shukrani zao za dhati kwa Benki ya Serikali ya TPB kwa kuwajali na kuwawezesha wafikie malengo yao ambayo walikuwa hawajakamilisha wakati wanastaafu.
Meneja wa TPB Mkoa wa Shinyanga Ndg Jumanne Wagana akitoa Elimu kwa Waalimu Wastaafu wilayani ya Kahama.
Walimu Wastaafu wakifuatilia kwa umakini Wawezeshaji kutoka Benki ya TPB wakitoa elimu ya fedha, mikopo na ujasiriamali.
Social Plugin