Rais Donald Trump wa Marekani ameonya kuwa nchi yake itayashambulia haraka na vikali maeneo 52 ya Iran iwapo Jamhuri hiyo ya Kiislam itafanya mashambulizi dhidi ya raia wa Marekani na mali zake kulipiza kisasi kwa mauaji ya Jenerali Qassem Soleimani.
Katika ujumbe wa kitisho kupitia ukurasa wa Twitter, Trump amesema maeneo yatakayolengwa ni yale yaliyo muhimu kwa Iran na utamaduni wake na kuonya Marekani haiko tayari kuendelea kutishwa na Iran.
Ujumbe huo wa Trump unafutia onyo la makundi ya wanamgambo yanayoiunga mkono Iran la kuvishambulia vituo vya Marakani nchini Iraq kutokana na mauaji ya kamanda huyo muhimu wa jeshi la Iran.
Katika ishara za mwanzo za uwezekano wa kulipa kisasi, makombora mawili yalilipiga eneo lililo karibu na ubalozi wa Marekani mjini Baghdad siku ya Jumamosi.
Makombora mengine mawili yaliishambulia kambi ya kijeshi ambayo inahifadhi wanajeshi wa Marekani lakini hakuna athari kubwa zilizoripotiwa.
....targeted 52 Iranian sites (representing the 52 American hostages taken by Iran many years ago), some at a very high level & important to Iran & the Iranian culture, and those targets, and Iran itself, WILL BE HIT VERY FAST AND VERY HARD. The USA wants no more threats!— Donald J. Trump (@realDonaldTrump) January 4, 2020
Social Plugin