Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAKULIMA GEITA WAIOMBA KAMPUNI YA PETROBENA KUNUNUA TUMBAKU



Picha ya pamoja Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini, Dk Titus Kamani akiwa na wajumbe wa mkutano wa MBCU pamoja na viongozi waandamizi wa kampuni ya uzambaziji pembejeo za kilimo ya Petrobena
Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini, Dk Titus Kamani akizungumza na wanachama wa chama kikuu cha Ushirika Mbogwe na Bukombe (MBCU)
Baadhi ya wanachama wa chama kikuuu cha ushirika (MBCU) wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini, Dk Titus Kamani.
Mkuu wa wilaya ya Mbogwe Matha Julius Mkupas akiwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa MBCU


Na Salvatory Ntandu - Malunde 1 blog Mbogwe

Wakulima wa zao la Tumbaku katika wilaya za Mbogwe na Bukombe mkoani Geita wameiomba kampuni ya usambazaji wa Pembejeo za kilimo ya Petrobena kuanza ununuzi wa zao hilo kwenye AMCOS tatu ambazo zilikosa wanunuzi wa zao hilo baada ya kampuni ya Tanzania Leaf Tobacco Company Limited (TLTC) kusitsha ununuzi wa zao hilo katika msimu uliopita.

Ombi hilo limetolewa jana na Catherin Agostino mkulima wa Tumbaku kutoka Wilaya ya Bukombe katika Mkutano mkuu wa Chama kikuuu cha Ushirika Mbogwe na Bukombe (MBCU) kilichofanyika jana wilayani Mbogwe na kuhudhuriwa na wajumbe mbalimbali wa AMCOS 35 zilizopo katika Ushirika huo.

“Tangu Kampuni ya TLTC imesitisha ununuzi wa Tumbaku wakulima wengi wamekata tamaa ya kuendelea na kilimo hiki kutokana na kukosa mnunuzi tunaiomba kampuni ya Petrobena kukubali kununua mazao yetu ili tuweze kuendeleza familia zetu”,alisema Agostino.

Aliongeza kuwa kama wameweza kusambaza Pembejeo kwa wakulima wote hapa nchini kwa wakati na kuondoa urasimu uliokuwepo hapo awali wa kuchelewa kwa pembejeo na kusababisha wakulima kushindwa kulima kwa tija na kujikuta wameingia katika madeni makubwa ambayo hayawezi kulipika kwa haraka.

“Taarifa tulizonazo sisi wakulima wa Mbogwe na Bukombe ni kuwa kampuni ya PETROBENA msimu wa kilimo wa 2019/20 imefunga mkataba na AMCOS ya ngokolo iliyopo katika chama kikuu cha ushirika kahama (KACU) kwaajili ya kununua tumbaku hivyo tunaimbani ombi letu watalifanyia kazi”,alisema Agostino.

Akitolea Ufafanuzi suala hilo Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini, Dk Titus Kamani alisema kuwa serikali ya awamu ya Tano imehakikisha kero za wakulima zinapatiwa ufumbuzi ikiwemo suala la masoko ya mazao kwa kutafuta kampuni mbalimbali za ununuzi ambapo kwa mwaka huu vyama vyote vilivyokuwa vinalima tumbaku zimepata wanunuzi.

“Mbogwe na Bukombe mmepata wanunuzi katika zao la Tumbaku na Pamba changamoto iliyojitokeza mwaka huu ni kwamba baadhi ya taasisi za kifedha zimegoma kutoa mikopo kwa kampuni ya Grand Tobacco limite ambayo mmefunga nayo mkataba na AMCOS zetu sisi kama serikali tutalifanyika kazi na mtapata majibu kwa haraka”,alisema Dk Kamani.

Pia Dk. Kamani aliwataka pia viongozi wa vyama vikuu na AMCOS kuhakikisha wanatenga fedha kwaaajili ya kununulia pembejeo katika msimu ujao wa kilimo wa 2020/21 ili kuondokana  na mikopo kutoka katika taasisi za kifedha ambayoimekuwa na riba kubwa isiyokuwa na tija kwa Wakulima.

Dk. Kamani aliwataka viongozi wa AMCOS zote zilizaopo katika mkoa wa Geita kuhakikisha wanajiunga na chama kikuu cha ushirika Mbogwe na Bukombe (MBCU) ili wawezekusaidiwa kwa ukaribu na serikali kupita viongozi wao pindi wanapopata matatizo sambamba na kupata huduma zingine ikiwepo mikopo ya pembejeo za kilimo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com