Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAKULIMA WA TUMBAKU URAMBO WAITAJA PETROBENA KUONGEZA UZALISHAJI KWA MWAKA 2019/2020

WAKULIMA wa zao la tumbaku wa chama kikuu cha ushirika cha Milambo kilichopo wilayani Urambo Mkoani Tabora wameipongeza Kampuni ya usambazaji pembejeo ya Petrobena kwa kuwarahisishia upatikanaji wa mbolea na madawa hali ambayo imesababisha kuongeza uzalishaji wa zao hilo katika msimu wa 2019/2020.

Hayo yamebainishwa na baadhi ya wakulima wa chama hicho Abisai Kasenge Zacharia William na Mathew Luzagila ,katika kikao cha Mkutano Mkuu wa pili mkuatano amabo umeafanyika katika ukumbi wa Kanisa Katoliki wilayani Urambo.

Wamesema msimu uliopita wamepata mafanikio makubwa ya zao hilo kutokana na kampuni ya Petrobena kusambaza pembejeo za mbolea na Madawa ya Mimea kwa wakati katika vyama vyao.

Wameongeza kuwa kabla ya kuwepo kwa kampuni ya Petrobena wakulima wengi walikuwa wakipata shida kucheleweshewa pembejeo za mbolea na madawa hali ambayo ilikuwa ikifanya zao lao la Tumbaku kuharibika.

Aidha Wakulima hao wamewataka mawakala wengine wa usambazaji pembejeo kuwa waaminifu kwa kuiga mwenendo wa kampuni ya Petrobena ili kuweza kumsaidia mkulima wa zao la Tumbaku kuzalisha kwa wingi zao hilo.

Hata hivyo Wakulima hao wameongeza kwa kusema kuwa Petrobena mbali ya kuwa wakala wa usambaji pembejeo na Madawa ya mimea wameiomba kampuni hiyo kufikiria kuwa miongoni mwa makapuni ya ununuzi wa tumbaku hapa nchini kutokana na uwezo wao, weledi mkubwa na kujali maslahi ya mkulima wa tumbaku.

Nae Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika wa wakulima wa tumbaku cha Milambo Hassan Magola amesema dhamira ya chama hicho ni kuendelea kutetea na kusimamia haki za wakulima wake ili wainuke kiuchumi.

Kaimu Mrajisi wa Vyama wa Ushirika Tanzania Benson Mlyege amewataka viongozi wa vyama vya ushirika kuwa waaminifu na kuwasilisha taarifa ya mali za vyama vyao, thamani ya mali hizo na mahali zilipo ili kuepuka ubadhirifu na wizi katika vyama vya ushirika .

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania Titus Kamani, amevitaka vyama vya ushirika hapa nchini kuhakikisha viongozi wa vyama vya msingi na wakulima wanapewa elimu ya ushirika na kilimo bora ili kufanya kilimo kiwe na tija katika maeneo yao.

Kamani amewaonya viongozi wa vyama vya ushirika wanaotaka kujitajirisha haraka kupitia jasho la mkulima kuacha mara moja tabia hiyo huku Akiwatahadrisha wale wasioridhika na hali zao kujiondoa mara moja katika vyama hivyo kabla hawajaondolewa.

MATUKIO KATIKA PICHA:

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com