Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania leo Ijumaa Januari 31, 2020 umempongeza Rais John Magufuli baada ya Rais Magufuli kueleza kuwa uchaguzi mkuu wa Oktoba, 2020 utakuwa huru na wa haki.
Mbali na pongeza hizo, ubalozi huo umetaka kuharakishwa kwa uanzishwaji wa tume huru ya uchaguzi.
“Tunatoa wito wa kuharakishwa kwa zoezi la uandikishaji wapiga kura lenye uwazi, kuanzishwa kwa tume huru ya uchaguzi na kuteuliwa mapema kwa waangalizi wa uchaguzi wa kitaifa na wa kimataifa wa kuaminika watakaofuatilia uchaguzi kwa kipindi kirefu na kipindi kifupi,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.
Ubalozi huo pia umesema unatarajia kuwepo kwa uchaguzi wa amani ambao wagombea wote watakutana kwa amani wakieleza mawazo yao na kampeni zitakazofanyika katika misingi ya usawa.
Januari 21, 2020 Rais Magufuli aliwahakikishia mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania kuwa uchaguzi huo utakuwa huru na wa haki, alipokuwa akizungumza nao Ikulu Dar es Salaam.
Social Plugin