Serikali ya uingereza hii leo imetoa onyo kwa raia wake kutosafiri kuelekea Iraq au kufanya safari za aina yoyote kuelekea Iran kufuatia kuuwawa kwa Qassem Soleimani, Kamanda wa kijeshi wa ngazi ya juu wa Iran.
Ofisi ya Wizara ya mambo ya kigeni imesema kufuatia mvutano wa kikanda unaozidi kupamba moto, hivi sasa imewashauri raia wake kutosafiri kuelekea katika maeneo hayo isipokuwa tu eneo la Kurdistan.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza Dominic Raab amesema ni vizuri raia wa taifa hilo kufikiria kwa makini iwapo ni salama kwao kusafiri kuelekea Iran kwa sasa.
Social Plugin