Meneja wa Shirika la Reli Kanda ya Kaskazini (TRC) Ramadhani Ebrahim Gombo akizungumza na waandishi wa habari Jijini Tanga kuhusu kurejea kwa treni ya mizigo
MBUNGE wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajab akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea eneo la reli ambalo liliathirika kwa kusombwa na maji Muheza ambalo kwa sasa limekarabatiwa na kuanza kupitisha treni
MBUNGE
wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajab akizungumza na waandishi wa
habari mara baada ya kutembelea eneo la reli ambalo liliathirika kwa
kusombwa na maji Muheza ambalo kwa sasa limekarabatiwa na kuanza
kupitisha treni
MBUNGE
wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajab katikati aliyevaa tisheti ya mistari nyeupe akiangalia ukarabati huo ukiwa unamalizika kuendelea eneo la Muheza ambapo kwa sasa Reli zimeanza kupita
Mafundi wa shirika la Reli mkoa wa Tanga wakiendelea na ukarabati huo
Greda likiendea na kazi eneo la reli Muheza kama lilivyokutwa
Greda likiendea na kazi eneo la reli Muheza kama lilivyokutwa
HATIMAYE usafirishaji wa mizigo kwa njia ya reli kutoka mkoa wa Tanga kwenye mikoa ya Kanda ya Kaskazini umerejea kwenye hali yake ya kawaida baada ya kukwama kwa kipindi cha miezi mitatu
Hatua hiyo inatokana na daraja kubwa lililopo eneo la Muheza kusombwa na maji mwishoni mwa mwaka jana wakati wa mvua kubwa zilizokuwa zikinyesha hapa nchini na hivyo kuleta athari kubwa.
Hayo yalisemwa jana na Meneja wa Shirika la Reli Kanda ya Kaskazini (TRC) Ramadhani Ebrahim Gombo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema usafiri huo umerejea baada ya kufanyia matengenezo makubwa kwenye eneo hilo.
Alisema kwamba baada ya daraja kubwa la reli lililopo eneo la Muheza kukatika lilishindwa kutumika na hivyo wafanyabiashara kushindwa kuitumia kwa ajili ya kusafirishia bidhaa zao na hivyo kusimama kwa muda.
“Daraja la Muheza lilisombwa na Maji Octoba 10 mwaka jana na ulazimika kuanza kunyia ukarabati kuanzia mwezi wa 11 tulianza kurekebisha kwa kuondoa maji eneo hilo kuwawezesha wananchi kuendelea na shughuli zao”Alisema
“Lakini baada ya hapo tulihamia maeneo mengine Korogwe,Mnyuzi, Gendagenda kwani maeneo mengi yaliathirika na tulivyomaliza maeneo hayo 23 Novemba 2019 ndipo tuliporudi hapa muheza mpaka Januari mwaka huu tulipomaliza daraja hilo na kwa sasa treni zinatembea na usafirishaji mizigo umerudi kwenye hali yake ya kawaida”Alisema
Alisema kwa sasa treni inaendelea vizuri na usafirishaji wa mizigo umerudi kwenye hali yake ya kawaida huku akielezwa kwamba wamepata hasara kubwa kwani treni za mizigo hazikufanya kazi ya kusafirisha mizigo na mzigo wa mingi wanategemea kutoka Bohari ya Mafuta mkoani Tanga (GBP) na Saruji kwenda mikoa ya Kilimanjaro, Dar na mikoa mingine Kanda ya Ziwa wamepata hasara kubwa kwa kusombwa daraja la muheza.
Hata hivyo Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu ambaye alitembelea eneo la reli wilayani Muheza ambalo lililikuwa limeathirika na mvua kubwa na kupelekea usafiri huo kusitishwa.
Alisema kwamba athari ambazo zimetokea kutokana na kusitishwa usafiri huo ni kubwa kwa sababu daraja hilo la reli na maeneo yote yalijaa maji na mawasiliana ya reli dar kwenda Tanga kukatika.
Aidha alisema lakini sasa shirika la reli wamefanya kazi nzuri sana kwa kipindi kifupi wamekuwa wakifanya kazi kwa usiku na mchana kuhakikisha inafanya kazi.
Mbunge huyo alisema kwamba kuanzia juzi wananchi wa Muheza wamejisikia furaha kubwa baada ya kuanza kuona reli inapita licha ya kupatikana kwa hasara kutokana na huduma hiyo kusitizwa kutokana na mvua kubwa zilizokuwa zikinyesha mwaka jana na kuleta athari hiyo.
“Kama juzi juzi mmesikia reli inapita kwenda Moshi lakini pia ilikuwa ipite na hapo Muheza kwenda Tanga lakini kutokana na tatizo hilo imeshindwa kufika huku lakini naamini serikali itaanzisha usafiri wa kuelekea mkoani Tanga kwa sasa baada ya matengenezo “Alisema
Social Plugin