Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

UTEUZI WA MAKATIBU TAWALA WA WILAYA


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika kwa mamlaka aliyokasimiwa kwa mujibu wa Sheria amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wa Wilaya nane (8) kwa kuwapandisha vyeo Makatibu Tarafa na kuwabadilisha vituo vya kazi Makatibu Tawala watatu (3).

Walioteuliwa ni wafuatao;
1.Michael J. Semindu – Kituo, Wilaya ya Mbalali 

2.Mikidadi D. Nchunguye – Kituo, Wilaya ya Kigoma 
3.Lincoln Tamba – Kituo, Wilaya ya Mlele 
4.Neema M. Nyalege – Kituo, Wilaya ya Kiteto 
5.Estomih M. Kyando – Kituo, Wilaya ya Iringa 

6.Hoffman H. Sanga – Kituo, Wilaya ya Mvomero
7.Amin M. Mrisho – Kituo, Wilaya ya Mwanga 


8. Nicodemus M. Shirima – Kituo, Wilaya ya Bariadi

Waliobadilishwa vituo vya kazi ni wafuatao;
1.Veronica Kinyemi – kutoka Wilaya ya Bariadi kwenda Wilaya ya Mkuranga 

2.Delmina M. Tumaini – Kutoka Wilaya ya Mkuranga kwenda Wilaya ya Kigamboni 
3.Rahel Mhando – Kutoka Wilaya ya Kigamboni kwenda  Wilaya ya Korogwe 

Wateule wapya waripoti Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora siku ya Jumanne tarehe 04 Februari, 2020 kwa ajili ya kukamilisha taratibu za Uteuzi.

  Dkt. Laurean I. P. Ndumbaro
 KATIBU MKUU (UTUMISHI).
Tarehe 31 Januari, 2020



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com