Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasili visiwani Zanzibar kwa ziara ya kikazi.
Baada ya kuwasili visiwani humo Waziri Mkuu amepokelewa na Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi, Hassan Khatib Hassan na viongozi mbalimbali.
Waziri Mkuu amekutana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Baadae leo Waziri Mkuu anatarajiwa kufanya ziara katika mkoa wa Kusini Unguja, kuzindua mradi wa afya ya kijiji, kukagua ujenzi wa maabara ya sayansi ya shule ya sekondari Bwejuu, mradi wa kilimo cha kisasa na kuzindua huduma ya mama na mtoto katika eneo la Bambi.
Social Plugin