Waziri Mkuu wa Iraq Adel Abdul Mahdi ametoa taarifa akilaani shambulizi la roketi katika ubalozi wa Marekani kwenye eneo la Green Zone katikati mwa Baghdad.
Shambulizi hilo limetokea tena dhidi ya ubalozi wa nchi za nje, wakati roketi za Katyusha zilipotua ndani ya eneo la ubalozi wa Marekani.
Amekemea vikali muendelezo wa vitendo hivi vya kukiuka sheria ambavyo vinadhoofisha taifa na utawala.
Abdul Mahdi ambaye pia ni kamanda mkuu wa jeshi la Iraq, amesema amevielekeza vikosi vya Iraq kupeleka askari na kuwatafuta washambuliaji, pamoja na kuanzisha uchunguzi juu ya tukio hilo, ili kuwakamata wote waliorusha roketi.
Pia ameahidi kuwa serikali italinda balozi zote na kuchukua hatua za lazima kwa mujibu wa sheria.